Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Faith

543 mistari · 124 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe.

  2. Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini?

  3. Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?

  4. Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu.

  5. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite.

  6. Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.

  7. Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.

  8. Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

  9. Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia.

  10. Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

  11. Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?

  12. Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi.

  13. Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

  14. Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake.

  15. Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika.

  16. Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu.

  17. Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.

  18. Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.

  19. kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,

  20. watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo.

  21. Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

  22. Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima.

  23. Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara.

  24. Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, utanihuisha tena, kutoka vilindi vya dunia utaniinua tena.

  25. Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena.