Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Faith

543 mistari · 124 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. ili awaokoe na mauti, na kuwahifadhi wakati wa njaa.

  2. Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

  3. Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.

  4. Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, tunapoliweka tumaini letu kwako.

  5. Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.

  6. Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.

  7. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.

  8. Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

  9. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

  10. Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

  11. Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.

  12. Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.

  13. Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana, yeye ni ngome yao wakati wa shida.

  14. Bwana huwasaidia na kuwaokoa, huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, kwa maana wanamkimbilia.

  15. Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

  16. Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

  17. Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na

  18. Mungu wangu. Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; kwa hiyo nitakukumbuka kutoka nchi ya Yordani, katika vilele vya Hermoni, kutoka Mlima Mizari.

  19. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi. Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

  20. Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.

  21. Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.

  22. Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu.

  23. Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda.

  24. Lakini ninamwita Mungu, naye Bwana huniokoa.

  25. Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti yangu.