Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Faith: General references

147 mistari · 124 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.

  2. Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.

  3. Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,

  4. ili awaokoe na mauti, na kuwahifadhi wakati wa njaa.

  5. Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.

  6. Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.

  7. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.

  8. Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

  9. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

  10. Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

  11. Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.

  12. Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.

  13. Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao,

  14. ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

  15. Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake.

  16. Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.

  17. Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.

  18. Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu.

  19. Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu.

  20. “Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika Bwana, ambaye matumaini yake ni katika Bwana.

  21. Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji. Hauogopi wakati wa joto ujapo; majani yake ni mabichi daima. Hauna hofu katika mwaka wa ukame na hautaacha kuzaa matunda.”

  22. Yesu akawajibu, “Amin, nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ngʼoka, ukatupwe baharini,’ litafanyika.

  23. Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.”

  24. Yesu akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”

  25. Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!”