Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Despondency

79 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. wale wanaotamani kifo ambacho hakiji, wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,

  2. ambao hujawa na furaha, na hushangilia wafikapo kaburini?

  3. Kwa nini uhai hupewa mtu ambaye njia yake imefichika, ambaye Mungu amemzungushia boma?

  4. Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula; kusononeka kwangu kunamwagika kama maji.

  5. Lile nililokuwa naliogopa limenijia; lile nililokuwa ninalihofia limenipata.

  6. Sina amani, wala utulivu; sina pumziko, bali taabu tu.”

  7. Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, kama nikikitandika kitanda changu gizani,

  8. kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’

  9. liko wapi basi tarajio langu? Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?

  10. Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? Je, tutashuka pamoja mavumbini?”

  11. “Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena?

  12. Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

  13. Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

  14. Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake.

  15. Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru;

  16. hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa.

  17. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu.

  18. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu.

  19. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa.

  20. Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito.

  21. Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu.

  22. Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu.

  23. Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni,

  24. ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada.

  25. Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake.