Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Despondency

79 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Waisraeli wakamwambia Mose, “Tutakufa! Tumepotea, sote tumepotea!

  2. Yeyote akaribiaye Maskani ya Bwana atakufa. Je, sisi sote tutakufa?”

  3. Miongoni mwa mataifa hayo hamtapata raha wala mahali pa kupumzisha wayo wa mguu wenu. Huko Bwana atawapa mahangaiko ya mawazo, macho yaliyochoka kwa kungojea na moyo uliokata tamaa.

  4. Utaishi katika mahangaiko siku zote, ukiwa umejaa hofu usiku na mchana, wala hutakuwa kamwe na uhakika wa maisha yako.

  5. Wakati wa asubuhi utasema hivi, “Laiti ingekuwa jioni!” Jioni utasema, “Laiti ingekuwa asubuhi,” kwa sababu ya hofu ile itakayojaza moyo wako na vitu vile macho yako yatakavyoviona.

  6. Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

  7. Kisha akasema:

  8. “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule iliposemekana, ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’

  9. Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie.

  10. Giza na kivuli kikuu kiikalie tena; wingu na likae juu yake; weusi na uifunike nuru yake.

  11. Usiku ule na ushikwe na giza kuu; usihesabiwe katika siku za mwaka, wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote.

  12. Usiku ule na uwe tasa; sauti ya furaha na isisikike ndani yake.

  13. Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku, wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.

  14. Nyota zake za alfajiri na ziwe giza; nao ungojee mwanga bila mafanikio, wala usiuone mwonzi wa kwanza wa mapambazuko,

  15. kwa sababu huo usiku haukunifungia mlango wa tumbo la mama yangu, ili kuyaficha macho yangu kutokana na taabu.

  16. “Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?

  17. Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea na matiti ili nipate kunyonyeshwa?

  18. Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani. Ningekuwa nimelala na kupumzika

  19. pamoja na wafalme na washauri wa dunia, waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,

  20. pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu, waliozijaza nyumba zao kwa fedha.

  21. Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu, kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?

  22. Huko waovu huacha kusumbua na huko waliochoka hupumzika.

  23. Wafungwa nao hufurahia utulivu wao, hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.

  24. Wadogo na wakubwa wamo humo, na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake.

  25. “Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni, na hao wenye uchungu kupewa uhai,