Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Afflictions and Adversities

526 mistari · 5 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

  2. “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu, ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.

  3. Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu, aweke mkono wake juu yetu sote wawili,

  4. mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

  5. Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.

  6. “Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza?

  7. “Kama akija na kukufunga gerezani, na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?

  8. Hakika utaisahau taabu yako, utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita.

  9. Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri, nalo giza litakuwa kama alfajiri.

  10. Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini; utatazama pande zote na kupumzika kwa salama.

  11. Utalala, wala hakuna atakayekuogofya, naam, wengi watajipendekeza kwako.

  12. Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza.

  13. Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.

  14. Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.

  15. Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.

  16. Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.

  17. Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni.

  18. Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

  19. Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.

  20. Huwamwagia dharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu.

  21. Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.

  22. Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.

  23. Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.

  24. Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; huwafanya wapepesuke kama walevi.

  25. Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.