Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Afflictions and Adversities: Despondency in

28 mistari · 5 vipengele

Mistari kuhusu Despondency in

Chuja kwa kitabu
  1. Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, nawe unashuka moyo; imekupiga wewe, nawe unafadhaika.

  2. Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, siamini kama angenisikiliza.

  3. Yeye angeniangamiza kwa dhoruba na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.

  4. Asingeniacha nipumue bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.

  5. Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?

  6. Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

  7. “Ingawa mimi sina kosa, haileti tofauti katika nafsi yangu; nauchukia uhai wangu.

  8. Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema, ‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’

  9. Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula, yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.

  10. Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu, yeye huwafunga macho mahakimu wake. Kama si yeye, basi ni nani?

  11. “Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji; zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.

  12. Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo, mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.

  13. Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu, nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’

  14. bado ninahofia mateso yangu yote, kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.

  15. Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, kwa nini basi nitaabishwe bure?

  16. Hata kama ningejiosha kwa sabuni na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

  17. wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

  18. “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu, ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.

  19. Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu, aweke mkono wake juu yetu sote wawili,

  20. mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

  21. Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.

  22. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi. Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?

  23. Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi.

  24. Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo!

  25. Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?