Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Afflictions and Adversities

526 mistari · 5 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.

  2. Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa.

  3. Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima.

  4. “Kwa habari yako wewe, kama ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda na kufanya yote nikuamuruyo, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu,

  5. Nitakiimarisha kiti chako cha enzi kama nilivyoagana na Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala juu ya Israeli.’

  6. “Lakini kama ukigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,

  7. ndipo nitakapoingʼoa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.

  8. Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini Bwana amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’

  9. Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ”

  10. na kusema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi, nami nitaondoka uchi, Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa, jina la Bwana litukuzwe.”

  11. Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, nawe unashuka moyo; imekupiga wewe, nawe unafadhaika.

  12. Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, wala udhia hauchipui kutoka ardhini.

  13. Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu.

  14. “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake.

  15. Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika.

  16. Yeye huipa nchi mvua, huyapeleka maji kunyesha mashamba.

  17. Huwainua juu wanyonge, nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama.

  18. Huipinga mipango ya wenye hila, ili mikono yao isifikie ufanisi.

  19. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali.

  20. Giza huwapata wakati wa mchana; wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku.

  21. Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu.

  22. Kwa hiyo maskini analo tarajio, nao udhalimu hufumba kinywa chake.

  23. “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.

  24. Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya.

  25. Kutoka majanga sita atakuokoa; naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.