Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 25:9takriban 1452 KK

    Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu 24,000.

  2. Hesabu 25:10takriban 1452 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  3. Hesabu 25:11takriban 1452 KK

    “Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza.

  4. Hesabu 25:12takriban 1452 KK

    Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye.

  5. Hesabu 25:13takriban 1452 KK

    Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.”

  6. Hesabu 25:14takriban 1452 KK

    Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.

  7. Hesabu 25:15takriban 1452 KK

    Jina la mwanamke wa Kimidiani aliyeuawa ni Kozbi binti wa Suri, aliyekuwa mkuu wa kabila la jamaa ya Wamidiani.

  8. Hesabu 25:16takriban 1452 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  9. Hesabu 25:17takriban 1452 KK

    “Watendeeni Wamidiani kama adui na mwaue,

  10. Hesabu 25:18takriban 1452 KK

    kwa sababu wao waliwatendea kama adui wakati waliwadanganya katika tukio la Peori na dada yao Kozbi, binti wa kiongozi wa Kimidiani, mwanamke ambaye aliuawa wakati tauni ilikuja kama matokeo ya tukio la Peori.”

  11. Hesabu 26:1takriban 1452 KK

    Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni,

  12. Hesabu 26:2takriban 1452 KK

    “Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.”

  13. Hesabu 26:3takriban 1452 KK

    Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema,

  14. Hesabu 26:4takriban 1452 KK

    “Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.” Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:

  15. Hesabu 26:5takriban 1452 KK

    Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki; kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

  16. Hesabu 26:6takriban 1452 KK

    kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.

  17. Hesabu 26:7takriban 1452 KK

    Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

  18. Hesabu 26:8takriban 1452 KK

    Mwana wa Palu alikuwa Eliabu,

  19. Hesabu 26:9takriban 1452 KK

    nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana.

  20. Hesabu 26:10takriban 1452 KK

    Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.

  21. Hesabu 26:11takriban 1452 KK

    Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.

  22. Hesabu 26:12takriban 1452 KK

    Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli; kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini; kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;

  23. Hesabu 26:13takriban 1452 KK

    kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera; kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.

  24. Hesabu 26:14takriban 1452 KK

    Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.

  25. Hesabu 26:15takriban 1452 KK

    Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni; kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi; kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;