Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 23:14takriban 1452 KK

    Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

  2. Hesabu 23:15takriban 1452 KK

    Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati ninapokwenda kuonana na Mungu kule.”

  3. Hesabu 23:16takriban 1452 KK

    Bwana akakutana na Balaamu, akaweka ujumbe katika kinywa chake akasema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”

  4. Hesabu 23:17takriban 1452 KK

    Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamuuliza, “Je, Bwana amesema nini?”

  5. Hesabu 23:18takriban 1452 KK

    Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake: “Balaki, inuka na usikilize, nisikie mimi, wewe mwana wa Sipori.

  6. Hesabu 23:19takriban 1452 KK

    Mungu si mtu, hata aseme uongo, wala yeye si mwanadamu, hata ajute. Je, anasema, kisha asitende? Je, anaahidi, asitimize?

  7. Hesabu 23:20takriban 1452 KK

    Nimepokea agizo kubariki; amebariki, nami siwezi kubadilisha.

  8. Hesabu 23:21takriban 1452 KK

    “Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, wala taabu katika Israeli. Bwana, Mungu wao yu pamoja nao, nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.

  9. Hesabu 23:22takriban 1452 KK

    Mungu aliwatoa kutoka Misri; wao wana nguvu za nyati.

  10. Hesabu 23:23takriban 1452 KK

    Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo, wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli. Sasa itasemwa kuhusu Yakobo na Israeli, ‘Tazama yale Mungu aliyotenda!’

  11. Hesabu 23:24takriban 1452 KK

    Taifa lainuka kama simba jike; linajiinua kama simba ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake na kunywa damu ya mawindo yake.”

  12. Hesabu 23:25takriban 1452 KK

    Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa!”

  13. Hesabu 23:26takriban 1452 KK

    Balaamu akajibu, “Je, sikukuambia ni lazima nifanye lolote analosema Bwana?”

  14. Hesabu 23:27takriban 1452 KK

    Basi Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo, nikupeleke mahali pengine. Huenda itampendeza Mungu kukuruhusu unilaanie hao watu kutoka mahali hapo.”

  15. Hesabu 23:28takriban 1452 KK

    Balaki akamchukua Balaamu juu ya Mlima Peori, unaotazamana na nyika.

  16. Hesabu 23:29takriban 1452 KK

    Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, uandae mafahali saba na kondoo dume saba kwa ajili yangu.”

  17. Hesabu 23:30takriban 1452 KK

    Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, kisha akatoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

  18. Hesabu 24:1takriban 1452 KK

    Basi Balaamu alipoona imempendeza Bwana kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.

  19. Hesabu 24:2takriban 1452 KK

    Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake,

  20. Hesabu 24:3takriban 1452 KK

    naye akatoa ujumbe wake: “Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori, ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

  21. Hesabu 24:4takriban 1452 KK

    ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu, ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi, ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka:

  22. Hesabu 24:5takriban 1452 KK

    “Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo, maskani yako, ee Israeli!

  23. Hesabu 24:6takriban 1452 KK

    “Kama mabonde, yanaenea, kama bustani kando ya mto, kama miti ya udi iliyopandwa na Bwana, kama mierezi kando ya maji.

  24. Hesabu 24:7takriban 1452 KK

    Maji yatatiririka kutoka ndoo zake; mbegu yake itakuwa na maji tele. “Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi; ufalme wake utatukuka.

  25. Hesabu 24:8takriban 1452 KK

    “Mungu alimleta kutoka Misri; yeye ana nguvu kama nyati. Anayararua mataifa yaliyo adui zake, na kuvunja mifupa yao vipande vipande; huwachoma kwa mishale yake.