Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 26:16takriban 1452 KK

    kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;

  2. Hesabu 26:17takriban 1452 KK

    kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.

  3. Hesabu 26:18takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.

  4. Hesabu 26:19takriban 1452 KK

    Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

  5. Hesabu 26:20takriban 1452 KK

    Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela; kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi; kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.

  6. Hesabu 26:21takriban 1452 KK

    Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.

  7. Hesabu 26:22takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.

  8. Hesabu 26:23takriban 1452 KK

    Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola; kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;

  9. Hesabu 26:24takriban 1452 KK

    kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu; kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.

  10. Hesabu 26:25takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.

  11. Hesabu 26:26takriban 1452 KK

    Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi; kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni; kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.

  12. Hesabu 26:27takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.

  13. Hesabu 26:28takriban 1452 KK

    Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

  14. Hesabu 26:29takriban 1452 KK

    Wazao wa Manase: kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi); kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.

  15. Hesabu 26:30takriban 1452 KK

    Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi: kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri; kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;

  16. Hesabu 26:31takriban 1452 KK

    kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli; kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;

  17. Hesabu 26:32takriban 1452 KK

    kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida; kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.

  18. Hesabu 26:33takriban 1452 KK

    (Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)

  19. Hesabu 26:34takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.

  20. Hesabu 26:35takriban 1452 KK

    Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao: kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela; kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri; kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;

  21. Hesabu 26:36takriban 1452 KK

    Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela: kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.

  22. Hesabu 26:37takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.

  23. Hesabu 26:38takriban 1452 KK

    Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela; kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli; kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;

  24. Hesabu 26:39takriban 1452 KK

    kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu; kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.

  25. Hesabu 26:40takriban 1452 KK

    Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa: kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi; kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.