Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 26:41takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.

  2. Hesabu 26:42takriban 1452 KK

    Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao: kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani:

  3. Hesabu 26:43takriban 1452 KK

    Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.

  4. Hesabu 26:44takriban 1452 KK

    Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna; kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi; kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;

  5. Hesabu 26:45takriban 1452 KK

    kutoka kwa wazao wa Beria: kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi; kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.

  6. Hesabu 26:46takriban 1452 KK

    (Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

  7. Hesabu 26:47takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

  8. Hesabu 26:48takriban 1452 KK

    Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli; kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;

  9. Hesabu 26:49takriban 1452 KK

    kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri; kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.

  10. Hesabu 26:50takriban 1452 KK

    Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.

  11. Hesabu 26:51takriban 1452 KK

    Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.

  12. Hesabu 26:52takriban 1452 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  13. Hesabu 26:53takriban 1452 KK

    “Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina.

  14. Hesabu 26:54takriban 1452 KK

    Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.

  15. Hesabu 26:55takriban 1452 KK

    Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao.

  16. Hesabu 26:56takriban 1452 KK

    Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”

  17. Hesabu 26:57takriban 1452 KK

    Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao: kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni; kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi; kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.

  18. Hesabu 26:58takriban 1452 KK

    Hizi pia zilikuwa koo za Walawi: ukoo wa Walibni; ukoo wa Wahebroni; ukoo wa Wamahli; ukoo wa Wamushi; ukoo wa wana wa Kora. (Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu;

  19. Hesabu 26:59takriban 1452 KK

    jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu.

  20. Hesabu 26:60takriban 1452 KK

    Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.

  21. Hesabu 26:61takriban 1452 KK

    Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)

  22. Hesabu 26:62takriban 1452 KK

    Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.

  23. Hesabu 26:63takriban 1452 KK

    Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

  24. Hesabu 26:64takriban 1452 KK

    Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai.

  25. Hesabu 26:65takriban 1452 KK

    Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.