Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 28:3takriban 1452 KK

    Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.

  2. Hesabu 28:4takriban 1452 KK

    Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni,

  3. Hesabu 28:5takriban 1452 KK

    kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ya mafuta ya zeituni.

  4. Hesabu 28:6takriban 1452 KK

    Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

  5. Hesabu 28:7takriban 1452 KK

    Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu.

  6. Hesabu 28:8takriban 1452 KK

    Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

  7. Hesabu 28:9takriban 1452 KK

    “ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta.

  8. Hesabu 28:10takriban 1452 KK

    Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.

  9. Hesabu 28:11takriban 1452 KK

    “ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.

  10. Hesabu 28:12takriban 1452 KK

    Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa, uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta;

  11. Hesabu 28:13takriban 1452 KK

    pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwa Bwana.

  12. Hesabu 28:14takriban 1452 KK

    Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini, na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka.

  13. Hesabu 28:15takriban 1452 KK

    Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Bwana kama sadaka ya dhambi.

  14. Hesabu 28:16takriban 1452 KK

    “ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana.

  15. Hesabu 28:17takriban 1452 KK

    Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu.

  16. Hesabu 28:18takriban 1452 KK

    Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida.

  17. Hesabu 28:19takriban 1452 KK

    Leteni mbele za Bwana sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

  18. Hesabu 28:20takriban 1452 KK

    Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa;

  19. Hesabu 28:21takriban 1452 KK

    pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa.

  20. Hesabu 28:22takriban 1452 KK

    Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu.

  21. Hesabu 28:23takriban 1452 KK

    Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi.

  22. Hesabu 28:24takriban 1452 KK

    Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayo Bwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

  23. Hesabu 28:25takriban 1452 KK

    Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

  24. Hesabu 28:26takriban 1452 KK

    “ ‘Siku ya malimbuko, mnapomletea Bwana sadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

  25. Hesabu 28:27takriban 1452 KK

    Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.