Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Marko 1:30takriban 27 BK

    Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Yesu habari zake.

  2. Marko 1:31takriban 27 BK

    Hivyo Yesu akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia.

  3. Marko 1:32takriban 27 BK

    Jioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Yesu wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu.

  4. Marko 1:33takriban 27 BK

    Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo.

  5. Marko 1:34takriban 27 BK

    Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.

  6. Marko 1:35takriban 27 BK

    Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Yesu akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba.

  7. Marko 1:36takriban 27 BK

    Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta,

  8. Marko 1:37takriban 27 BK

    nao walipomwona, wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta!”

  9. Marko 1:38takriban 27 BK

    Yesu akawajibu, “Twendeni mahali pengine kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia, kwa sababu hicho ndicho nilichokuja kukifanya.”

  10. Marko 1:39takriban 27 BK

    Kwa hiyo akazunguka Galilaya kote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu.

  11. Marko 1:40takriban 27 BK

    Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Yesu, akamwomba akipiga magoti, akamwambia, “Ukitaka, waweza kunitakasa.”

  12. Marko 1:41takriban 27 BK

    Yesu, akiwa amejawa na huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!”

  13. Marko 1:42takriban 27 BK

    Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika.

  14. Marko 1:43takriban 27 BK

    Baada ya Yesu kumwonya vikali, akamruhusu aende zake

  15. Marko 1:44takriban 27 BK

    akimwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”

  16. Marko 1:45takriban 27 BK

    Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Yesu hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi lakini alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.

  17. Marko 2:1takriban 31 BK

    Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani.

  18. Marko 2:2takriban 31 BK

    Hivyo watu wengi wakakusanyika kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno.

  19. Marko 2:3takriban 31 BK

    Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne.

  20. Marko 2:4takriban 31 BK

    Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa Yesu kwa ajili ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa mahali pale alipokuwa Yesu, wakamshusha yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.

  21. Marko 2:5takriban 31 BK

    Yesu alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”

  22. Marko 2:6takriban 31 BK

    Basi baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wameketi huko wakawaza mioyoni mwao,

  23. Marko 2:7takriban 31 BK

    “Kwa nini mtu huyu anasema hivi? Huyu anakufuru! Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”

  24. Marko 2:8takriban 31 BK

    Mara moja Yesu akatambua rohoni mwake kile walichokuwa wanawaza mioyoni mwao, naye akawaambia, “Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu?

  25. Marko 2:9takriban 31 BK

    Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’?