circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Marko 3:7takriban 31 BK
Yesu pamoja na wanafunzi wake wakaondoka huko wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya ukamfuata.
- Marko 3:8takriban 31 BK
Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, umati mkubwa wa watu ukamjia kutoka Uyahudi, Yerusalemu, Idumaya, na ngʼambo ya Yordani, pamoja na wale wa sehemu za karibu na Tiro na Sidoni.
- Marko 3:9takriban 31 BK
Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga.
- Marko 3:10takriban 31 BK
Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa.
- Marko 3:11takriban 31 BK
Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
- Marko 3:12takriban 31 BK
Lakini aliwaonya wasimseme yeye ni nani.
- Marko 3:13takriban 31 BK
Yesu akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia.
- Marko 3:14takriban 31 BK
Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri
- Marko 3:15takriban 31 BK
na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.
- Marko 3:16takriban 31 BK
Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro);
- Marko 3:17takriban 31 BK
Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo);
- Marko 3:18takriban 31 BK
Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
- Marko 3:19takriban 31 BK
na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.
- Marko 3:20takriban 31 BK
Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula.
- Marko 3:21takriban 31 BK
Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”
- Marko 3:22takriban 31 BK
Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!”
- Marko 3:23takriban 31 BK
Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani?
- Marko 3:24takriban 31 BK
Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
- Marko 3:25takriban 31 BK
Nayo nyumba kama ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
- Marko 3:26takriban 31 BK
Naye Shetani kama akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama bali mwisho wake umewadia.
- Marko 3:27takriban 31 BK
Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali zake.
- Marko 3:28takriban 31 BK
Amin, nawaambia, dhambi zote na makufuru yote ya wanadamu watasamehewa.
- Marko 3:29takriban 31 BK
Lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.”
- Marko 3:30takriban 31 BK
Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”
- Marko 3:31takriban 31 BK
Kisha wakaja ndugu zake Yesu pamoja na mama yake. Wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita.