Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Marko 4:22takriban 31 BK

    Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni.

  2. Marko 4:23takriban 31 BK

    Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

  3. Marko 4:24takriban 31 BK

    Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi.

  4. Marko 4:25takriban 31 BK

    Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.”

  5. Marko 4:26takriban 31 BK

    Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.

  6. Marko 4:27takriban 31 BK

    Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo.

  7. Marko 4:28takriban 31 BK

    Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke.

  8. Marko 4:29takriban 31 BK

    Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.”

  9. Marko 4:30takriban 31 BK

    Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza?

  10. Marko 4:31takriban 31 BK

    Ni kama punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini.

  11. Marko 4:32takriban 31 BK

    Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye matawi yake.”

  12. Marko 4:33takriban 31 BK

    Kwa mifano mingine mingi kama hii Yesu alinena nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulielewa.

  13. Marko 4:34takriban 31 BK

    Hakusema nao neno lolote pasipo mfano. Lakini alipokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.

  14. Marko 4:35takriban 31 BK

    Siku hiyo ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni twende mpaka ngʼambo.”

  15. Marko 4:36takriban 31 BK

    Wakauacha ule umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua nyingine nyingi pamoja naye.

  16. Marko 4:37takriban 31 BK

    Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji.

  17. Marko 4:38takriban 31 BK

    Yesu alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”

  18. Marko 4:39takriban 31 BK

    Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, “Uwe kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa.

  19. Marko 4:40takriban 31 BK

    Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?”

  20. Marko 4:41takriban 31 BK

    Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”

  21. Marko 5:1takriban 31 BK

    Wakafika upande wa pili wa ziwa wakaingia katika nchi ya Wagerasi.

  22. Marko 5:2takriban 31 BK

    Yesu alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini akakutana naye.

  23. Marko 5:3takriban 31 BK

    Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo.

  24. Marko 5:4takriban 31 BK

    Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia.

  25. Marko 5:5takriban 31 BK

    Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.