Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Marko 5:6takriban 31 BK

    Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia, akapiga magoti mbele yake.

  2. Marko 5:7takriban 31 BK

    Akapiga kelele kwa nguvu akisema, “Una nini nami, Yesu, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!”

  3. Marko 5:8takriban 31 BK

    Kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe pepo mchafu!”

  4. Marko 5:9takriban 31 BK

    Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tuko wengi.”

  5. Marko 5:10takriban 31 BK

    Akamsihi Yesu sana asiwapeleke nje ya nchi ile.

  6. Marko 5:11takriban 31 BK

    Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima.

  7. Marko 5:12takriban 31 BK

    Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu wakisema, “Tuamuru twende kwenye wale nguruwe. Turuhusu tuwaingie.”

  8. Marko 5:13takriban 31 BK

    Basi Yesu akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao 2,000, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.

  9. Marko 5:14takriban 31 BK

    Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakatoka kwenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia.

  10. Marko 5:15takriban 31 BK

    Walipofika kwa Yesu, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu legioni akiwa ameketi hapo, amevaa nguo na mwenye akili timamu. Wakaogopa.

  11. Marko 5:16takriban 31 BK

    Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine yaliyomtokea yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu, na habari za lile kundi la nguruwe pia.

  12. Marko 5:17takriban 31 BK

    Basi watu wakaanza kumwomba Yesu aondoke katika nchi yao.

  13. Marko 5:18takriban 31 BK

    Yesu alipokuwa anaingia kwenye mashua, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu akamsihi Yesu waende pamoja.

  14. Marko 5:19takriban 31 BK

    Yesu hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokuhurumia.”

  15. Marko 5:20takriban 31 BK

    Yule mtu akaenda zake, akaanza kutangaza katika Dekapoli mambo makuu Yesu aliyomtendea. Nao watu wote wakastaajabu.

  16. Marko 5:21takriban 31 BK

    Yesu alipokwisha kuvuka tena na kufika ngʼambo, umati mkubwa wa watu ukamzunguka yeye akiwa hapo kando ya bahari.

  17. Marko 5:22takriban 31 BK

    Kisha mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Yesu, akapiga magoti miguuni pake,

  18. Marko 5:23takriban 31 BK

    akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye atakuwa hai.”

  19. Marko 5:24takriban 31 BK

    Hivyo Yesu akaenda pamoja naye. Umati mkubwa wa watu ukamfuata, nao watu wakawa wanamsonga.

  20. Marko 5:25takriban 31 BK

    Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili.

  21. Marko 5:26takriban 31 BK

    Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya.

  22. Marko 5:27takriban 31 BK

    Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake,

  23. Marko 5:28takriban 31 BK

    kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.”

  24. Marko 5:29takriban 31 BK

    Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.

  25. Marko 5:30takriban 31 BK

    Ghafula Yesu akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akaugeukia ule umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”