Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 28:5takriban 1491 KK

    Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi.

  2. Kutoka 28:6takriban 1491 KK

    “Tengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi.

  3. Kutoka 28:7takriban 1491 KK

    Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kisibau.

  4. Kutoka 28:8takriban 1491 KK

    Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri.

  5. Kutoka 28:9takriban 1491 KK

    “Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli

  6. Kutoka 28:10takriban 1491 KK

    kufuatana na walivyozaliwa: majina sita katika kito kimoja, na mengine sita katika kito kingine.

  7. Kutoka 28:11takriban 1491 KK

    Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu,

  8. Kutoka 28:12takriban 1491 KK

    na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za Bwana.

  9. Kutoka 28:13takriban 1491 KK

    Tengeneza vijalizo vya dhahabu

  10. Kutoka 28:14takriban 1491 KK

    na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo.

  11. Kutoka 28:15takriban 1491 KK

    “Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa.

  12. Kutoka 28:16takriban 1491 KK

    Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili.

  13. Kutoka 28:17takriban 1491 KK

    Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi;

  14. Kutoka 28:18takriban 1491 KK

    katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi;

  15. Kutoka 28:19takriban 1491 KK

    safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto;

  16. Kutoka 28:20takriban 1491 KK

    na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu.

  17. Kutoka 28:21takriban 1491 KK

    Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.

  18. Kutoka 28:22takriban 1491 KK

    “Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba.

  19. Kutoka 28:23takriban 1491 KK

    Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake, uzifungie kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani.

  20. Kutoka 28:24takriban 1491 KK

    Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete zilizo katika pembe za hicho kifuko cha kifuani,

  21. Kutoka 28:25takriban 1491 KK

    nazo zile ncha nyingine za mkufu zifunge kwenye vile vijalizo viwili, na uzishikamanishe na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele.

  22. Kutoka 28:26takriban 1491 KK

    Tengeneza pete mbili za dhahabu, uzishikamanishe kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau.

  23. Kutoka 28:27takriban 1491 KK

    Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uzishikamanishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau.

  24. Kutoka 28:28takriban 1491 KK

    Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa kwenye pete zile za kisibau kwa kamba ya buluu, ziunganishwe na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau.

  25. Kutoka 28:29takriban 1491 KK

    “Wakati wowote Aroni aingiapo Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi kama kumbukumbu ya kudumu mbele za Bwana.