Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 28:30takriban 1491 KK

    Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele za Bwana. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana.

  2. Kutoka 28:31takriban 1491 KK

    “Shona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu,

  3. Kutoka 28:32takriban 1491 KK

    na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike.

  4. Kutoka 28:33takriban 1491 KK

    Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, na uweke pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga.

  5. Kutoka 28:34takriban 1491 KK

    Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka upindo wa joho lile.

  6. Kutoka 28:35takriban 1491 KK

    Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za Bwana, ili asije akafa.

  7. Kutoka 28:36takriban 1491 KK

    “Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana.

  8. Kutoka 28:37takriban 1491 KK

    Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba.

  9. Kutoka 28:38takriban 1491 KK

    Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa Bwana.

  10. Kutoka 28:39takriban 1491 KK

    “Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi.

  11. Kutoka 28:40takriban 1491 KK

    Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima.

  12. Kutoka 28:41takriban 1491 KK

    Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

  13. Kutoka 28:42takriban 1491 KK

    “Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani.

  14. Kutoka 28:43takriban 1491 KK

    Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.

  15. Kutoka 29:1takriban 1491 KK

    “Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo dume wawili wasio na dosari.

  16. Kutoka 29:2takriban 1491 KK

    Kutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate midogo myembamba.

  17. Kutoka 29:3takriban 1491 KK

    Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo dume wawili.

  18. Kutoka 29:4takriban 1491 KK

    Kisha mlete Aroni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji.

  19. Kutoka 29:5takriban 1491 KK

    Chukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi.

  20. Kutoka 29:6takriban 1491 KK

    Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba.

  21. Kutoka 29:7takriban 1491 KK

    Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake.

  22. Kutoka 29:8takriban 1491 KK

    Walete wanawe na uwavike makoti,

  23. Kutoka 29:9takriban 1491 KK

    pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe.

  24. Kutoka 29:10takriban 1491 KK

    “Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake.

  25. Kutoka 29:11takriban 1491 KK

    Mchinje huyo fahali mbele za Bwana kwenye mlango wa Hema la Kukutania.