circa AD 48–96
Letters to the Churches
Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.
Mistari ya kipindi hiki
- Wakolosai 3:14takriban 64 BK
Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.
- Wakolosai 3:15takriban 64 BK
Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.
- Wakolosai 3:16takriban 64 BK
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.
- Wakolosai 3:17takriban 64 BK
Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.
- Wakolosai 3:18takriban 64 BK
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana.
- Wakolosai 3:19takriban 64 BK
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.
- Wakolosai 3:20takriban 64 BK
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.
- Wakolosai 3:21takriban 64 BK
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
- Wakolosai 3:22takriban 64 BK
Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.
- Wakolosai 3:23takriban 64 BK
Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu,
- Wakolosai 3:24takriban 64 BK
kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia.
- Wakolosai 3:25takriban 64 BK
Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.
- Wakolosai 4:1takriban 64 BK
Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni.
- Wakolosai 4:2takriban 64 BK
Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru.
- Wakolosai 4:3takriban 64 BK
Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.
- Wakolosai 4:4takriban 64 BK
Ombeni ili nipate kuitangaza Injili kwa udhahiri kama ipasavyo kunena.
- Wakolosai 4:5takriban 64 BK
Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
- Wakolosai 4:6takriban 64 BK
Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.
- Wakolosai 4:7takriban 64 BK
Tikiko atawaambia habari zangu zote. Yeye ni ndugu mpendwa, mtendakazi mwaminifu na mtumishi mwenzangu katika Bwana.
- Wakolosai 4:8takriban 64 BK
Nimemtuma kwenu kwa madhumuni haya ili mpate kufahamu hali yetu, na pia awatie moyo.
- Wakolosai 4:9takriban 64 BK
Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa na mwaminifu, ambaye ni mmoja wenu. Watawaambia mambo yote yanayotendeka hapa kwetu.
- Wakolosai 4:10takriban 64 BK
Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni.)
- Wakolosai 4:11takriban 64 BK
Yesu, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.
- Wakolosai 4:12takriban 64 BK
Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti.
- Wakolosai 4:13takriban 64 BK
Ninashuhudia kumhusu kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na wale wa Hierapoli.