Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waefeso 6:19takriban 64 BK

    Niombeeni na mimi pia, ili kila nifunguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri,

  2. Waefeso 6:20takriban 64 BK

    ambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni ili nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo.

  3. Waefeso 6:21takriban 64 BK

    Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa.

  4. Waefeso 6:22takriban 64 BK

    Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali yetu, na awatie moyo.

  5. Waefeso 6:23takriban 64 BK

    Amani iwe kwa ndugu, na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.

  6. Waefeso 6:24takriban 64 BK

    Neema iwe na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo wa dhati. Amen.

  7. Wafilipi 1:1takriban 64 BK

    Waraka wa Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu: Kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu walioko Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi:

  8. Wafilipi 1:2takriban 64 BK

    Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

  9. Wafilipi 1:3takriban 64 BK

    Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi.

  10. Wafilipi 1:4takriban 64 BK

    Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha,

  11. Wafilipi 1:5takriban 64 BK

    kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo.

  12. Wafilipi 1:6takriban 64 BK

    Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Kristo Yesu.

  13. Wafilipi 1:7takriban 64 BK

    Ni haki na ni wajibu wangu kufikiri hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninyi mko moyoni mwangu. Ikiwa nimefungwa au nikiwa ninaitetea na kuithibitisha Injili, ninyi nyote mnashiriki neema ya Mungu pamoja nami.

  14. Wafilipi 1:8takriban 64 BK

    Mungu ni shahidi wangu jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote kwa huruma ya Kristo Yesu.

  15. Wafilipi 1:9takriban 64 BK

    Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote,

  16. Wafilipi 1:10takriban 64 BK

    ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo,

  17. Wafilipi 1:11takriban 64 BK

    mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu.

  18. Wafilipi 1:12takriban 64 BK

    Basi, ndugu zangu, nataka mjue kwamba mambo yale yaliyonipata kwa kweli yamesaidia sana kueneza Injili.

  19. Wafilipi 1:13takriban 64 BK

    Matokeo yake ni kwamba imejulikana wazi kwa walinzi wote wa jumba la kifalme na kwa wengine wote kuwa nimefungwa kwa ajili ya Kristo.

  20. Wafilipi 1:14takriban 64 BK

    Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga.

  21. Wafilipi 1:15takriban 64 BK

    Ni kweli kwamba wengine wanamhubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana, lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema.

  22. Wafilipi 1:16takriban 64 BK

    Hawa wa mwisho wanamhubiri Kristo kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba nimo humu gerezani kwa ajili ya kuitetea Injili.

  23. Wafilipi 1:17takriban 64 BK

    Hao wa kwanza wanamtangaza Kristo kutokana na tamaa zao wenyewe wala si kwa moyo mweupe, bali wanakusudia kuongeza mateso yangu katika huku kufungwa kwangu.

  24. Wafilipi 1:18takriban 64 BK

    Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema, Kristo anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi. Naam, nami nitaendelea kufurahi,

  25. Wafilipi 1:19takriban 64 BK

    kwa maana ninajua kwamba kwa maombi yenu na kwa msaada unaotolewa na Roho wa Yesu Kristo, yale yaliyonipata mimi yatageuka kuwa wokovu wangu.