Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Mercy of God

102 mistari · 36 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;

  2. Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

  3. Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  4. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.

  5. Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako.

  6. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  7. Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  8. Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  9. Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  10. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  11. Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako.

  12. Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.

  13. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

  14. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.

  15. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.

  16. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele.

  17. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  18. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.

  19. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.

  20. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele.

  21. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele.

  22. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele.

  23. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.

  24. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.

  25. Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.