Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Mercy of God: Everlasting

30 mistari · 36 vipengele

Mistari kuhusu Everlasting

Chuja kwa kitabu
  1. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  2. Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara.

  3. Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  4. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.

  5. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

  6. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.

  7. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.

  8. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele.

  9. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  10. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.

  11. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.

  12. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele.

  13. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele.

  14. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele.

  15. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.

  16. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.

  17. Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  18. Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele.

  19. Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  20. Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele.

  21. Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.

  22. Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.

  23. Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele.

  24. Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele.

  25. Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele.