Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.

  2. Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

  3. Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

  4. Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:

  5. “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

  6. Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”

  7. Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”

  8. Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

  9. Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

  10. kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku,

  11. kwa zeze yenye nyuzi kumi na kwa sauti ya kinubi.

  12. Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

  13. Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!

  14. Mjinga hafahamu, mpumbavu haelewi,

  15. ingawa waovu huchipua kama majani na wote watendao mabaya wanastawi, wataangamizwa milele.

  16. Bali wewe, Ee Bwana, utatukuzwa milele.

  17. Ee Bwana, hakika adui zako, hakika adui zako wataangamia. Wote watendao mabaya watatawanyika.

  18. Umeitukuza pembe yangu kama ile ya nyati dume, mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.

  19. Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.

  20. Wenye haki watastawi kama mtende, watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,

  21. waliopandwa katika nyumba ya Bwana, watastawi katika nyua za Mungu wetu.

  22. Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

  23. wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.”

  24. Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.

  25. Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele.