Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, Ee Mungu Mwokozi wetu, tumaini la miisho yote ya duniani na la bahari zilizo mbali sana,

  2. uliyeumba milima kwa uwezo wako, ukiwa umejivika nguvu,

  3. uliyenyamazisha dhoruba za bahari, ngurumo za mawimbi yake, na ghasia za mataifa.

  4. Wale wanaoishi mbali sana wanaogopa maajabu yako, kule asubuhi ipambazukiapo na kule jioni inakofifilia umeziita nyimbo za furaha.

  5. Waitunza nchi na kuinyeshea, waitajirisha kwa wingi. Vijito vya Mungu vimejaa maji ili kuwapa watu nafaka, kwa maana wewe umeviamuru.

  6. Umeilowesha mifereji yake na kusawazisha kingo zake; umeilainisha kwa manyunyu na kuibariki mimea yake.

  7. Umeuvika mwaka taji ya baraka, magari yako yanafurika kwa wingi.

  8. Mbuga za majani za jangwani umezineemesha; vilima vimevikwa furaha.

  9. Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama, na mabonde yamepambwa kwa mavuno; vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.

  10. Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,

  11. ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote.

  12. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

  13. Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia.

  14. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

  15. Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

  16. Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

  17. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

  18. Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu.

  19. Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.

  20. Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!”

  21. Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Bwana, usikawie.

  22. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo. Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu.

  23. Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki.

  24. Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

  25. Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.