Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati Mungu arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!

  2. Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.

  3. Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.

  4. Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.

  5. Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.

  6. Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.

  7. Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.

  8. Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.

  9. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Njiwa mkimya wa mbali.” Utenzi wa Daudi. Baada ya kukamatwa na Wafilisti huko Gathi. Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao.

  10. Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, wengi wananishambulia kwa kiburi chao.

  11. Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe.

  12. Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini?

  13. Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga shauri la kunidhuru.

  14. Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu.

  15. Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa.

  16. Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?

  17. Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu.

  18. Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Bwana, ambaye neno lake ninalisifu,

  19. katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

  20. Ee Mungu, nina nadhiri kwako, nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani.

  21. Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili niweze kuenenda mbele za Mungu katika nuru ya uzima.

  22. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite.

  23. Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.

  24. Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.

  25. Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali.