Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Paul: Is taken to Rome in custody of Julius, a centurion, and guard of soldiers; takes shipping, accompanied by other prisoners, and sails by way of the coasts of Asia; stops at Sidon, and at Myra

5 mistari · 103 vipengele

Mistari kuhusu Is taken to Rome in custody of Julius, a centurion, and guard of soldiers; takes shipping, accompanied by other prisoners, and sails by way of the coasts of Asia; stops at Sidon, and at Myra

  1. Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa njia ya bahari kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa kiongozi mmoja wa askari aliyeitwa Juliasi, aliyekuwa wa Kikosi cha Walinzi wa Kaisari.

  2. Tulipanda meli iliyotoka Adramitio, iliyokuwa inakaribia kusafiri kwenda kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia, tukaanza safari yetu tukiwa pamoja na Aristarko, Mmakedonia kutoka Thesalonike.

  3. Kesho yake tukatia nanga Sidoni, naye Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kwa rafiki zake ili wamtimizie mahitaji yake.

  4. Kutoka huko tukaingia baharini tena na tukapita upande wa chini wa kisiwa cha Kipro kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.

  5. Baada ya sisi kuvuka bahari iliyoko upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira huko Likia.