Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Paul: Visits Coos, Rhodes, Patara; takes ship for Tyre; tarries at Tyre seven days; is brought on his way by the disciples to the outskirts of the city; kneels down and prays; takes ship; comes to Ptolemais; salutes the brethren, and abides one day

7 mistari · 103 vipengele

Mistari kuhusu Visits Coos, Rhodes, Patara; takes ship for Tyre; tarries at Tyre seven days; is brought on his way by the disciples to the outskirts of the city; kneels down and prays; takes ship; comes to Ptolemais; salutes the brethren, and abides one day

  1. Tulipokwisha kujitenga nao, tukaanza safari kwa njia ya bahari moja kwa moja mpaka Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukaenda Patara.

  2. Hapo tukapata meli iliyokuwa inavuka kwenda Foinike tukapanda tukasafiri nayo.

  3. Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.

  4. Baada ya kuwatafuta wanafunzi wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale wanafunzi wakiongozwa na Roho wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu.

  5. Lakini muda wetu ulipokwisha, tukaondoka tukaendelea na safari yetu. Wale wanafunzi pamoja na wake zao na watoto wakatusindikiza hadi nje ya mji. Wote tukapiga magoti pale pwani tukaomba.

  6. Baada ya kuagana, tukapanda melini, nao wakarudi majumbani mwao.

  7. Tukaendelea na safari yetu toka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu ndugu wa huko, tukakaa nao kwa siku moja.