Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Parents

156 mistari · 48 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake.

  2. kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.

  3. Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake.

  4. Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru.

  5. Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki.

  6. Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe, bali yeye ampendaye huwa mwangalifu kumwadibisha.

  7. Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa.

  8. Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini, usiwe mshirika katika mauti yake.

  9. Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee.

  10. Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

  11. Usimnyime mtoto adhabu, ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa.

  12. Mwadhibu kwa fimbo na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini.

  13. Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau.

  14. Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake.

  15. Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako.

  16. Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

  17. Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa, mumewe pia humsifu, akisema:

  18. Hutajumuika nao kwenye mazishi, kwa kuwa umeharibu nchi yako na kuwaua watu wako. Mzao wa mwovu hatatajwa tena kamwe.

  19. Walio hai, walio hai: hao wanakusifu, kama ninavyofanya leo. Baba huwaambia watoto wao habari za uaminifu wako.

  20. “Je, mama aweza kumsahau mtoto aliyeko matitini mwake akinyonya, wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, mimi sitakusahau wewe!

  21. Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana, wao na wazao wao pamoja nao.

  22. Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”

  23. Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.”

  24. “Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli nao watakuwa watu wangu,” asema Bwana.

  25. Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao. Wajane wako pia wanaweza kunitumaini mimi.”