Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Obedience

136 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

  2. Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.

  3. Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako.

  4. Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.

  5. Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako.

  6. Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.

  7. Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.

  8. Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

  9. Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.

  10. Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki.

  11. Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.

  12. Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.

  13. Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii.

  14. Ee Bwana, ninangojea wokovu wako, nami ninafuata amri zako,

  15. Ninazitii sheria zako, kwa sababu ninazipenda mno.

  16. Nimetii mausia yako na sheria zako, kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.

  17. Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare.

  18. Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”

  19. Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake, bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.

  20. Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

  21. Kama mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi,

  22. lakini niliwapa amri hii nikisema: Nitiini mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa.

  23. “Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi.

  24. Nami kama nikimwambia mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ kisha akageuka kutoka dhambi yake na kufanya lile lililo haki na sawa,

  25. kama akirudisha kile alichochukua rehani kwa ajili ya deni, akarudisha alichoiba na kufuata amri zile ziletazo uzima, wala hafanyi uovu, hakika ataishi, hatakufa.