Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Obedience

136 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa.

  2. Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

  3. kwa wale walishikao agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake.

  4. Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake.

  5. Mhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.

  6. Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.

  7. Msifuni Bwana. Heri mtu yule amchaye Bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

  8. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.

  9. Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu.

  10. Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako!

  11. Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote.

  12. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.

  13. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.

  14. Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.

  15. Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.

  16. Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako.

  17. Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.

  18. Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe.

  19. Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho.

  20. Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele.

  21. Nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.

  22. Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako.

  23. Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.

  24. Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.

  25. Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.