Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Levites

186 mistari · 17 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. nikawatuma kwa Ido kiongozi huko Kasifia. Niliwaambia watakayomwambia Ido na ndugu zake, watumishi wa Hekalu huko Kasifia, ili waweze kutuletea wahudumu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu.

  2. Kwa sababu mkono wa neema wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, walituletea Sherebia, mtu mwenye uwezo kutoka wazao wa Mahli mwana wa Lawi, mwana wa Israeli, na wana wa Sherebia pamoja na ndugu zao wanaume kumi na wanane.

  3. Naye Hashabia, pamoja na Yeshaya kutoka wazao wa Merari na ndugu zake na wapwa wake wanaume ishirini.

  4. Vilevile walileta watumishi wa Hekalu 220, kikundi ambacho Daudi na maafisa walikuwa wamekiweka kusaidia Walawi. Wote walikuwa wameorodheshwa kwa majina.

  5. Baada ya mambo haya kutendeka, viongozi walinijia na kusema, “Watu wa Israeli, wakiwemo makuhani na Walawi, hawakujitenga na majirani zao katika kufanya machukizo, kama yale ya Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori.

  6. Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.”

  7. Miongoni mwa Walawi: Yozabadi, Shimei, Kelaya (ndiye Kelita), Pethahia, Yuda na Eliezeri.

  8. Kutoka waimbaji: Eliashibu. Kutoka mabawabu: Shalumu, Telemu na Uri.

  9. Walawi: wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74

  10. Waimbaji: wazao wa Asafu 148

  11. Mabawabu wa malango: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138

  12. Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

  13. wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,

  14. wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,

  15. wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,

  16. wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,

  17. wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,

  18. wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,

  19. wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

  20. wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

  21. wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

  22. wazao wa Nesia na Hatifa.

  23. Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,

  24. wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

  25. wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.