Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Levites: Religious zeal of

7 mistari · 17 vipengele

Mistari kuhusu Religious zeal of

  1. Kwa hiyo Mose akasimama kwenye ingilio la kambi, akasema, “Yeyote aliye upande wa Bwana, aje upande wangu.” Walawi wote wakamjia.

  2. Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ”

  3. Walawi wakafanya kama Mose alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao 3,000.

  4. Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake, ‘Mimi siwahitaji kamwe.’ Akawasahau jamaa zake, asiwatambue hata watoto wake, lakini akaliangalia neno lako na kulilinda Agano lako.

  5. Humfundisha Yakobo mausia yako na Israeli sheria yako. Hufukiza uvumba mbele zako na sadaka nzima za kuteketezwa juu ya madhabahu yako.

  6. Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

  7. “Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu.