Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Doubting

105 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mungu wangu. Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; kwa hiyo nitakukumbuka kutoka nchi ya Yordani, katika vilele vya Hermoni, kutoka Mlima Mizari.

  2. Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

  3. Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.

  4. Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.

  5. Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa.

  6. Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.

  7. “Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena?

  8. Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

  9. Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

  10. Kwa nini unasema, ee Yakobo, nanyi ee Israeli, kulalamika, “Njia yangu imefichwa Bwana asiione, Mungu wangu hajali shauri langu?”

  11. Je wewe, hufahamu? Je wewe, hujasikia? Bwana ni Mungu wa milele, Muumba wa miisho ya dunia. Hatachoka wala kulegea, wala hakuna hata mmoja awezaye kuupima ufahamu wake.

  12. Lakini Sayuni alisema, “Bwana ameniacha, Bwana amenisahau.”

  13. “Je, mama aweza kumsahau mtoto aliyeko matitini mwake akinyonya, wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, mimi sitakusahau wewe!

  14. “Tazama jinsi tumezungukwa na jeshi ili kuuteka mji huu. Kwa sababu ya upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo ambao wanaushambulia. Ulilosema limetokea kama vile unavyoona sasa.

  15. Ingawa mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo, wewe, Ee Bwana Mwenyezi, uliniambia, ‘Nunua shamba kwa fedha, na jambo hilo lishuhudiwe.’ ”

  16. Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata.

  17. Ghafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi.

  18. Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!”

  19. Naye Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nako kukawa shwari kabisa.

  20. Wale watu wakashangaa, wakisema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!”

  21. Yohana aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Kristo alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake

  22. ili wakamuulize, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

  23. Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu.

  24. Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

  25. Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”