Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Armies

207 mistari · 77 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. aliyefuata ni jemadari Yehohanani, akiwa na askari 280,000 walio tayari kwa vita;

  2. aliyefuata ni Amasia mwana wa Zikri, ambaye alijitolea kwa ajili ya kazi ya Bwana, akiwa na askari 200,000.

  3. Kutoka Benyamini: Eliada, askari shujaa akiwa na watu 200,000 wenye silaha za nyuta na ngao;

  4. aliyefuata ni Yehozabadi, akiwa na askari 180,000 wenye silaha za vita.

  5. Hawa ndio waliomtumikia mfalme, mbali na wale mfalme aliweka katika miji yenye ngome huko Yuda yote.

  6. Amazia akawaita watu wa Yuda pamoja, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia kufuatana na jamaa zao katika Yuda yote na Benyamini. Kisha akawahesabu wale wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na akakuta kwamba walikuwa wanaume 300,000 watu walio tayari kwa utumishi wa jeshi, walio na uwezo wa kutumia mkuki na ngao.

  7. Akawaajiri pia watu 100,000 wapiganaji kutoka Israeli kwa talanta 100 za fedha.

  8. Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi lililofunzwa vizuri, lililokuwa tayari kwenda vitani kwa vikosi kufuatana na idadi yao kama walivyokusanywa na Yeieli mwandishi na Maaseya msimamizi chini ya maelekezo ya Hanania, mmojawapo wa maafisa wa mfalme.

  9. Idadi yote ya viongozi wa jamaa waliowaongoza hawa wapiganaji walikuwa 2,600.

  10. Chini ya uongozi wao kulikuwa na jeshi la askari 307,500 watu waliofundishwa kwa ajili ya vita, jeshi lenye nguvu la kumsaidia mfalme dhidi ya adui zake.

  11. Uzia akalipatia jeshi lote ngao, mikuki, chapeo, dirii, pinde na mawe ya kombeo.

  12. Huko Yerusalemu watu wenye utaalamu mkubwa wakatengeneza mitambo iliyotumika katika minara na kwenye pembe za ulinzi ili kurusha mishale na kuvurumisha mawe makubwa. Sifa zake zikaenea mbali sana kwa sababu alisaidiwa mno mpaka akawa na nguvu sana.

  13. Wimbo. Zaburi ya Asafu. Ee Mungu, usinyamaze kimya, usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.

  14. Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.

  15. Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.

  16. Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”

  17. Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, wanafanya muungano dhidi yako,

  18. mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari,

  19. Gebali, Amoni na Amaleki, Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.

  20. Hata Ashuru wameungana nao kuwapa nguvu wazao wa Loti.

  21. Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini hapo kijito cha Kishoni,

  22. ambao waliangamia huko Endori na wakawa kama takataka juu ya nchi.

  23. Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, watawala wao kama Zeba na Salmuna,

  24. ambao walisema, “Na tumiliki nchi ya malisho ya Mungu.”

  25. Wakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramu, na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda.