Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Armies: Who were exempt from service in

9 mistari · 77 vipengele

Mistari kuhusu Who were exempt from service in

  1. Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine.

  2. Bwana alikuwa amemwambia Mose:

  3. “Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.

  4. Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka.

  5. Maafisa wataliambia jeshi: “Je, kuna yeyote aliyejenga nyumba mpya ambayo haijawekwa wakfu? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akaiweka wakfu.

  6. Je, kuna yeyote aliyepanda shamba la mizabibu na hajaanza kulifurahia? Yeye na arudi nyumbani, au sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akalifurahia.

  7. Je, kuna yeyote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.”

  8. Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.”

  9. Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.