Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Habakuki 2:16takriban 626 KK

    Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.

  2. Habakuki 2:17takriban 626 KK

    Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. Kwa sababu umemwaga damu ya mtu; umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.

  3. Habakuki 2:18takriban 626 KK

    “Sanamu ina thamani gani, kwani mwanadamu ndiye alichonga? Ama kinyago kinachofundisha uongo? Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.

  4. Habakuki 2:19takriban 626 KK

    Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’ Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’ Je, linaweza kuongoza? Limefunikwa kwa dhahabu na fedha; hakuna pumzi ndani yake.

  5. Habakuki 2:20takriban 626 KK

    Lakini Bwana yuko katika Hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze mbele yake.”

  6. Habakuki 3:1takriban 626 KK

    Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi.

  7. Habakuki 3:2takriban 626 KK

    Bwana, nimezisikia sifa zako; nami naogopa kwa matendo yako, Ee Bwana. Fufua kazi yako katikati ya miaka, katikati ya miaka tangaza habari yako; katika ghadhabu kumbuka rehema.

  8. Habakuki 3:3takriban 626 KK

    Mungu alitoka Temani, yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu, na sifa zake zikaifunika dunia.

  9. Habakuki 3:4takriban 626 KK

    Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa.

  10. Habakuki 3:5takriban 626 KK

    Tauni ilimtangulia; maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.

  11. Habakuki 3:6takriban 626 KK

    Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.

  12. Habakuki 3:7takriban 626 KK

    Niliona watu wa Kushani katika dhiki, na makazi ya Midiani katika maumivu makali.

  13. Habakuki 3:8takriban 626 KK

    Ee Bwana, uliikasirikia mito? Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? Je, ulighadhibikia bahari ulipoendesha farasi wako na magari yako ya ushindi?

  14. Habakuki 3:9takriban 626 KK

    Uliufunua upinde wako na kuita mishale mingi. Uliigawa dunia kwa mito;

  15. Habakuki 3:10takriban 626 KK

    milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu.

  16. Habakuki 3:11takriban 626 KK

    Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.

  17. Habakuki 3:12takriban 626 KK

    Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa.

  18. Habakuki 3:13takriban 626 KK

    Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo.

  19. Habakuki 3:14takriban 626 KK

    Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya, wakifurahi kama walio karibu kutafuna wale wanyonge waliokuwa mafichoni.

  20. Habakuki 3:15takriban 626 KK

    Ulikanyaga bahari kwa farasi wako, ukisukasuka maji makuu.

  21. Habakuki 3:16takriban 626 KK

    Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu, midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti; uchakavu ukanyemelea mifupa yangu, na miguu yangu ikatetemeka. Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa kuyajilia mataifa yaliyotuvamia.

  22. Habakuki 3:17takriban 626 KK

    Ingawa mtini hauchanui maua na hakuna zabibu juu ya mizabibu, ingawaje mzeituni hauzai, na hata mashamba hayatoi chakula, iwapo hakuna kondoo katika banda, wala ngʼombe katika zizi,

  23. Habakuki 3:18takriban 626 KK

    hata hivyo nitashangilia katika Bwana, nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

  24. Habakuki 3:19takriban 626 KK

    Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, huniwezesha kupita juu ya vilima. Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.

  25. Sefania 1:1takriban 630 KK

    Neno la Bwana lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda: