Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.”

  2. Mose alikuwa huko pamoja na Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.

  3. Kutoka 34:29takriban 1491 KK

    Mose alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa ukingʼaa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana.

  4. Kutoka 34:30takriban 1491 KK

    Aroni na Waisraeli wote walipomwona Mose, kuwa uso wake unangʼaa, waliogopa kumkaribia.

  5. Kutoka 34:31takriban 1491 KK

    Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao.

  6. Kutoka 34:32takriban 1491 KK

    Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai.

  7. Kutoka 34:33takriban 1491 KK

    Mose alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake.

  8. Kutoka 34:34takriban 1491 KK

    Lakini kila wakati Mose alipoingia mbele za Bwana kuzungumza naye, aliondoa ule utaji mpaka alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa,

  9. Kutoka 34:35takriban 1491 KK

    waliona kuwa uso wake unangʼaa. Kisha Mose angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na Bwana.

  10. Kutoka 35:1takriban 1491 KK

    Mose akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndiyo mambo ambayo Bwana amewaamuru ninyi mfanye:

  11. Kutoka 35:2takriban 1491 KK

    Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya kupumzika kwa Bwana. Yeyote atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe.

  12. Kutoka 35:3takriban 1491 KK

    Msiwashe moto mahali popote katika makazi yenu siku ya Sabato.”

  13. Kutoka 35:4takriban 1491 KK

    Mose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo Bwana aliloamuru:

  14. Kutoka 35:5takriban 1491 KK

    Toeni sadaka kwa Bwana kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea Bwana sadaka ya dhahabu, fedha na shaba;

  15. Kutoka 35:6takriban 1491 KK

    nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; singa za mbuzi;

  16. Kutoka 35:7takriban 1491 KK

    ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo; mbao za mshita;

  17. Kutoka 35:8takriban 1491 KK

    mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri;

  18. Kutoka 35:9takriban 1491 KK

    vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

  19. Kutoka 35:10takriban 1491 KK

    “Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Bwana alichoamuru:

  20. Kutoka 35:11takriban 1491 KK

    Maskani pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako;

  21. Kutoka 35:12takriban 1491 KK

    Sanduku la Agano pamoja na mipiko yake, kifuniko cha kiti cha rehema na pazia linalokizuia;

  22. Kutoka 35:13takriban 1491 KK

    meza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate ya Wonyesho;

  23. Kutoka 35:14takriban 1491 KK

    kinara cha taa kwa ajili ya mwanga pamoja na vifaa vyake vyote, taa na mafuta kwa ajili ya mwanga;

  24. Kutoka 35:15takriban 1491 KK

    madhabahu ya kufukiza uvumba pamoja na mipiko yake, mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri; pazia la mlangoni mahali pa kuingilia ndani ya maskani;

  25. Kutoka 35:16takriban 1491 KK

    madhabahu ya sadaka za kuteketeza pamoja na wavu wake wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote; sinia la shaba pamoja na tako lake;