Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 35:17takriban 1491 KK

    pazia la eneo la ua pamoja na nguzo zake na vitako vyake, pazia la ingilio la kwenye ua;

  2. Kutoka 35:18takriban 1491 KK

    vigingi vya hema kwa ajili ya maskani pamoja na ua na kamba zake;

  3. Kutoka 35:19takriban 1491 KK

    mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu kwa ajili ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.”

  4. Kutoka 35:20takriban 1491 KK

    Ndipo jumuiya yote ya Waisraeli ilipoondoka mbele ya Mose,

  5. Kutoka 35:21takriban 1491 KK

    na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa Bwana, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu.

  6. Kutoka 35:22takriban 1491 KK

    Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.

  7. Kutoka 35:23takriban 1491 KK

    Kila mmoja aliyekuwa na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi, au singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, au ngozi za pomboo, wakavileta.

  8. Kutoka 35:24takriban 1491 KK

    Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa Bwana, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta.

  9. Kutoka 35:25takriban 1491 KK

    Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi.

  10. Kutoka 35:26takriban 1491 KK

    Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi.

  11. Kutoka 35:27takriban 1491 KK

    Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kisibau na kwenye kifuko cha kifuani.

  12. Kutoka 35:28takriban 1491 KK

    Wakaleta pia vikolezi na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri.

  13. Kutoka 35:29takriban 1491 KK

    Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za Bwana kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya Bwana aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Mose.

  14. Kutoka 35:30takriban 1491 KK

    Kisha Mose akawaambia Waisraeli, “Tazameni, Bwana amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda,

  15. Kutoka 35:31takriban 1491 KK

    naye amemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, na uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi,

  16. Kutoka 35:32takriban 1491 KK

    ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba,

  17. Kutoka 35:33takriban 1491 KK

    kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi wa kupendeza.

  18. Kutoka 35:34takriban 1491 KK

    Tena amempa yeye pamoja na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, uwezo wa kufundisha wengine.

  19. Kutoka 35:35takriban 1491 KK

    Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zifanywazo na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari.

  20. Kutoka 36:1takriban 1491 KK

    Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu Bwana aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile Bwana alivyoagiza.”

  21. Kutoka 36:2takriban 1491 KK

    Ndipo Mose akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Bwana alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi.

  22. Kutoka 36:3takriban 1491 KK

    Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi.

  23. Kutoka 36:4takriban 1491 KK

    Ikafika wakati mafundi wote wenye ujuzi waliokuwa wakiifanya kazi yote ya mahali patakatifu wakasimamisha kazi zao,

  24. Kutoka 36:5takriban 1491 KK

    wakaja na kumwambia Mose, “Watu wanaleta vitu vingi kuliko tunavyohitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo Bwana ameagiza ifanyike.”

  25. Kutoka 36:6takriban 1491 KK

    Ndipo Mose akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi yote: “Mtu yeyote mwanaume au mwanamke asilete tena kitu chochote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu wakazuiliwa kuleta zaidi,