Skip to content

Hur

12 mistari · 25 wanafamilia

Mistari inayomtaja Hur

  1. Kwa hiyo Yoshua akapigana na Waamaleki kama Mose alivyomwagiza, nao Mose, Aroni na Huri wakapanda juu ya kilima.

  2. Mikono ya Mose ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Aroni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Mose, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama.

  3. Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”

  4. “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda,

  5. Kisha Mose akawaambia Waisraeli, “Tazameni, Bwana amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda,

  6. (Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu Bwana alichomwamuru Mose,

  7. Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri.

  8. Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.

  9. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa: Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu,

  10. Wana wa Yuda walikuwa: Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.

  11. Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.

  12. Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Bwana Mungu, hivyo Solomoni na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko.