Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 25:3takriban 1491 KK

    Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba;

  2. Kutoka 25:4takriban 1491 KK

    nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi;

  3. Kutoka 25:5takriban 1491 KK

    ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo; mbao za mshita;

  4. Kutoka 25:6takriban 1491 KK

    mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri;

  5. Kutoka 25:7takriban 1491 KK

    na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

  6. Kutoka 25:8takriban 1491 KK

    “Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao.

  7. Kutoka 25:9takriban 1491 KK

    Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.

  8. Kutoka 25:10takriban 1491 KK

    “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, upana wa dhiraa moja na nusu, na kimo cha dhiraa moja na nusu.

  9. Kutoka 25:11takriban 1491 KK

    Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka.

  10. Kutoka 25:12takriban 1491 KK

    Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine.

  11. Kutoka 25:13takriban 1491 KK

    Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu.

  12. Kutoka 25:14takriban 1491 KK

    Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba.

  13. Kutoka 25:15takriban 1491 KK

    Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa.

  14. Kutoka 25:16takriban 1491 KK

    Kisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa.

  15. Kutoka 25:17takriban 1491 KK

    “Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu.

  16. Kutoka 25:18takriban 1491 KK

    Tengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko.

  17. Kutoka 25:19takriban 1491 KK

    Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili.

  18. Kutoka 25:20takriban 1491 KK

    Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko.

  19. Kutoka 25:21takriban 1491 KK

    Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku.

  20. Kutoka 25:22takriban 1491 KK

    Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.

  21. Kutoka 25:23takriban 1491 KK

    “Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili, upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu.

  22. Kutoka 25:24takriban 1491 KK

    Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.

  23. Kutoka 25:25takriban 1491 KK

    Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne, na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote.

  24. Kutoka 25:26takriban 1491 KK

    Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne.

  25. Kutoka 25:27takriban 1491 KK

    Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza.