Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 25:28takriban 1491 KK

    Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza.

  2. Kutoka 25:29takriban 1491 KK

    Tengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka.

  3. Kutoka 25:30takriban 1491 KK

    Utaweka mikate ya Wonyesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima.

  4. Kutoka 25:31takriban 1491 KK

    “Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja.

  5. Kutoka 25:32takriban 1491 KK

    Matawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine.

  6. Kutoka 25:33takriban 1491 KK

    Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa.

  7. Kutoka 25:34takriban 1491 KK

    Juu ya kinara chenyewe vitakuwepo vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake.

  8. Kutoka 25:35takriban 1491 KK

    Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla.

  9. Kutoka 25:36takriban 1491 KK

    Matovu na matawi yote yatakuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakifuliwa kwa dhahabu safi.

  10. Kutoka 25:37takriban 1491 KK

    “Kisha tengeneza taa zake saba na uziweke juu ya kinara hicho ili ziangaze mbele yake.

  11. Kutoka 25:38takriban 1491 KK

    Mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote zitakuwa za dhahabu safi.

  12. Kutoka 25:39takriban 1491 KK

    Utatumia talanta moja ya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na vifaa vyake vyote.

  13. Kutoka 25:40takriban 1491 KK

    Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

  14. Kutoka 26:1takriban 1491 KK

    “Tengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo.

  15. Kutoka 26:2takriban 1491 KK

    Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane, na upana wa dhiraa nne

  16. Kutoka 26:3takriban 1491 KK

    Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano.

  17. Kutoka 26:4takriban 1491 KK

    Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.

  18. Kutoka 26:5takriban 1491 KK

    Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vielekeane.

  19. Kutoka 26:6takriban 1491 KK

    Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya Hema liwe kitu kimoja.

  20. Kutoka 26:7takriban 1491 KK

    “Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani.

  21. Kutoka 26:8takriban 1491 KK

    Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini, na upana wa dhiraa nne.

  22. Kutoka 26:9takriban 1491 KK

    Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya maskani.

  23. Kutoka 26:10takriban 1491 KK

    Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine.

  24. Kutoka 26:11takriban 1491 KK

    Kisha tengeneza vifungo hamsini vya shaba, uviingize katika vile vitanzi ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja.

  25. Kutoka 26:12takriban 1491 KK

    Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia la Hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaningʼinizwa upande wa nyuma wa Hema.