Rukia maudhui

circa 1050–1010 BC

Samuel & King Saul

Israel demands a king; Samuel anoints Saul, whose disobedience leads to his rejection as God chooses a man after his own heart.

810 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. 1 Samweli 30:10takriban 1056 KK

    kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia.

  2. 1 Samweli 30:11takriban 1056 KK

    Wakamkuta Mmisri katika shamba fulani, nao wakamleta kwa Daudi. Wakampa huyo Mmisri maji ya kunywa na chakula;

  3. 1 Samweli 30:12takriban 1056 KK

    kipande cha andazi la tini na andazi la zabibu zilizokaushwa. Akala naye akapata nguvu, kwa kuwa hakuwa amekula chakula chochote wala kunywa maji kwa siku tatu usiku na mchana.

  4. 1 Samweli 30:13takriban 1056 KK

    Daudi akamuuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?” Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita.

  5. 1 Samweli 30:14takriban 1056 KK

    Tulivamia Negebu ya Wakerethi, na nchi ya Yuda, na Negebu ya Kalebu. Nasi tulichoma moto Siklagi.”

  6. 1 Samweli 30:15takriban 1056 KK

    Daudi akamuuliza, “Je, unaweza kuniongoza kufikia kundi hili la uvamizi?” Akajibu, “Niapie mbele ya Mungu kwamba hutaniua wala kunikabidhi mikononi mwa bwana wangu, nami nitakupeleka hadi waliko.”

  7. 1 Samweli 30:16takriban 1056 KK

    Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda.

  8. 1 Samweli 30:17takriban 1056 KK

    Daudi akapigana nao kuanzia machweo ya jua hadi kesho yake jioni, na hakuna yeyote miongoni mwao aliyetoroka, isipokuwa vijana wanaume 400 waliopanda ngamia na kutoroka.

  9. 1 Samweli 30:18takriban 1056 KK

    Daudi akarudisha kila kitu Waamaleki walikuwa wamechukua, pamoja na wake zake wawili.

  10. 1 Samweli 30:19takriban 1056 KK

    Hakuna chochote kilichopotea: kijana au mzee, mvulana au msichana, nyara au kitu kingine chochote walichokuwa wamechukua. Daudi akarudisha kila kitu.

  11. 1 Samweli 30:20takriban 1056 KK

    Akachukua makundi yote ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, nao watu wake wakawaswaga wanyama hao mbele ya wanyama wengine wa kufugwa, wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.”

  12. 1 Samweli 30:21takriban 1056 KK

    Kisha Daudi akafika kwa wale watu 200 waliokuwa wamechoka sana kumfuata na ambao waliachwa nyuma kwenye Bonde la Besori. Wakatoka kwenda kumlaki Daudi na wale watu aliokuwa nao. Daudi na watu wake walipowakaribia, akawasalimu.

  13. 1 Samweli 30:22takriban 1056 KK

    Lakini watu wote waovu na wakorofi miongoni mwa wafuasi wa Daudi wakasema, “Kwa sababu hawakwenda pamoja nasi, hatutagawana nao nyara tulizorudisha. Lakini, kila mtu aweza kuchukua mkewe na watoto wake na kuondoka.”

  14. 1 Samweli 30:23takriban 1056 KK

    Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Bwana ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu.

  15. 1 Samweli 30:24takriban 1056 KK

    Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyekwenda vitani. Wote watashiriki sawa.”

  16. 1 Samweli 30:25takriban 1056 KK

    Daudi akafanya hili liwe amri na agizo kwa Israeli kutoka siku ile hata leo.

  17. 1 Samweli 30:26takriban 1056 KK

    Daudi alipofika Siklagi, akatuma baadhi ya nyara kwa wazee wa Yuda, waliokuwa rafiki zake, akasema, “Tazama, hapa kuna zawadi kwa ajili yenu kutoka nyara za adui za Bwana.”

  18. 1 Samweli 30:27takriban 1056 KK

    Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri;

  19. 1 Samweli 30:28takriban 1056 KK

    kwa wale walioko Aroeri, Sifmothi, Eshtemoa

  20. 1 Samweli 30:29takriban 1056 KK

    na Rakali; kwa wale waliokuwa katika miji ya Wayerameeli na ya Wakeni;

  21. 1 Samweli 30:30takriban 1056 KK

    na kwa wale walioko Horma, Bori-Ashani, Athaki,

  22. 1 Samweli 30:31takriban 1056 KK

    na kwa wakazi wa Hebroni; na kwa wale waliokuwa mahali pengine pote ambako Daudi na watu wake walitembelea.

  23. 1 Samweli 31:1takriban 1056 KK

    Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika Mlima Gilboa.

  24. 1 Samweli 31:2takriban 1056 KK

    Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua.

  25. 1 Samweli 31:3takriban 1056 KK

    Mapigano yakawa makali sana kumzunguka Sauli, nao wapiga upinde wakampata na kumjeruhi vibaya.