Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Wicked

724 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake.

  2. Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”

  3. Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia.

  4. Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

  5. Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.

  6. Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.

  7. Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Bwana unamzunguka mtu anayemtumaini.

  8. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana. Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.

  9. Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.

  10. Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.

  11. Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya.

  12. Zaburi ya Daudi. Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya,

  13. Waovu hula njama dhidi ya wenye haki na kuwasagia meno,

  14. kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Bwana humtegemeza mwenye haki.

  15. Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.

  16. Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.

  17. Lakini waovu wataangamia: Adui za Bwana watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi.

  18. Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.

  19. Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.

  20. Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni,

  21. lakini alitoweka mara na hakuonekana, ingawa nilimtafuta, hakupatikana.

  22. Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

  23. Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, mafanikio yao yatakatiliwa mbali.

  24. Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.

  25. Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.