Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Wicked

724 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ndipo huja mbele za watu na kusema, ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.

  2. Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’

  3. “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; mara mbili hata mara tatu,

  4. ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie.

  5. Yeye hajibu wakati watu waliapo kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

  6. Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; Mwenyezi hayazingatii.

  7. Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

  8. Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

  9. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.

  10. Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

  11. Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

  12. Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.

  13. Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya.

  14. Unawaangamiza wasemao uongo. Bwana huwachukia wamwagao damu na wadanganyifu.

  15. Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, mioyo yao imejaa maangamizi. Koo lao ni kaburi lililo wazi, kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.

  16. Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku.

  17. Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.

  18. Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.

  19. Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani.

  20. Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.

  21. Njia zake daima hufanikiwa; hujivuna na amri zako ziko mbali naye, huwacheka kwa dharau adui zake wote.

  22. Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, daima nitakuwa na furaha, kamwe sitakuwa na shida.”

  23. Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.

  24. Huvizia karibu na vijiji; kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, akivizia wapitaji.

  25. Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.