Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Wicked

724 mistari · 18 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?

  2. “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:

  3. Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha.

  4. Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.

  5. Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

  6. yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

  7. Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

  8. Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.

  9. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

  10. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.

  11. Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

  12. Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.

  13. Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.

  14. Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,

  15. anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,

  16. ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi,

  17. kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga.

  18. Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,

  19. kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri.

  20. Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, sasa inatokeza nje.

  21. Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.

  22. “Kama bado kuna malaika upande wake kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake,

  23. kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’:

  24. ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake.

  25. Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.