Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Righteousness of God

73 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, wewe ambaye umefanya mambo makuu. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?

  2. Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki mchana kutwa, kwa maana wale waliotaka kunidhuru, wameaibishwa na kufadhaishwa.

  3. Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri.

  4. Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

  5. Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi.

  6. Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.

  7. Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa.

  8. Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.

  9. Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana.

  10. itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.

  11. Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.

  12. Mbingu zinatangaza haki yake, na mataifa yote huona utukufu wake.

  13. Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

  14. vyote na viimbe mbele za Bwana, kwa maana yuaja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa haki.

  15. Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

  16. Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.

  17. Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

  18. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.

  19. Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.

  20. Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.

  21. Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.

  22. Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi.

  23. Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu.

  24. Haki yako ni ya milele, na sheria yako ni kweli.

  25. Sheria zako ni sahihi milele, hunipa ufahamu ili nipate kuishi.