Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Rich

145 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

  2. yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

  3. Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

  4. Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.

  5. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

  6. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.

  7. Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

  8. Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.

  9. “Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’

  10. kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu, ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata,

  11. basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa, kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana.

  12. Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka,

  13. kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye.

  14. Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,

  15. Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi amekwenda nyumbani kwa Ahimeleki.” Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? Kwa nini unajivuna mchana kutwa, wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?

  16. Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.

  17. Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli.

  18. Unapenda kila neno lenye kudhuru, ewe ulimi wenye hila!

  19. Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema yako, atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.

  20. Wenye haki wataona na kuogopa, watamcheka, wakisema,

  21. “Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

  22. Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

  23. Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu.

  24. Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.

  25. Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri.