Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Temptation

346 mistari · 52 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu.

  2. Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.

  3. Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.

  4. Kama Bwana asingelinisaidia upesi, ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.

  5. Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.

  6. Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.

  7. Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako.

  8. Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.

  9. Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao.

  10. Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

  11. tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

  12. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

  13. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

  14. Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao,

  15. kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu.

  16. Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona!

  17. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.

  18. Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda.

  19. Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,

  20. Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya,

  21. Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya.

  22. Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; achana nayo, na uelekee njia yako.

  23. Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

  24. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.

  25. Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,