Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Temptation: Resistance to temptation

121 mistari · 52 vipengele

Mistari kuhusu Resistance to temptation

Chuja kwa kitabu
  1. baada ya kitambo mke wa Potifa akamtamani Yosefu, akamwambia, “Njoo, ukutane nami kimwili!”

  2. Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi.

  3. Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?”

  4. Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yosefu siku baada ya siku, Yosefu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye.

  5. Lakini tulimwomba Mungu wetu, na tukaweka ulinzi usiku na mchana kupambana na tishio hili.

  6. “Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani.

  7. “Kama nimeishi katika uongo au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,

  8. Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, naye atajua kwamba sina hatia:

  9. kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia, kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu, au kama mikono yangu imetiwa unajisi,

  10. basi wengine na wale nilichokipanda, nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.

  11. “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke, au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,

  12. basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, nao wanaume wengine walale naye.

  13. Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, naam, dhambi ya kuhukumiwa.

  14. Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.

  15. “Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,

  16. nitafanya nini Mungu atakaponikabili? Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?

  17. Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, si ndiye aliwaumba? Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote ndani ya mama zetu?

  18. “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,

  19. kama nimekula chakula changu mwenyewe, bila kuwashirikisha yatima;

  20. kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo, au mtu mhitaji asiye na mavazi

  21. ambaye wala moyo wake haukunibariki kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu,

  22. na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima, nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,

  23. basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, nao na uvunjike kutoka kiungio chake.

  24. Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu, nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo.

  25. “Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’